KNUT yaandamana Makueni

Maafisa wa Muungano wa Kitaifa wa Walimu, KNUT tawi la Makueni, wameandamana katika mji wa Wote wakitaka Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti hiyo, Lydia Mutegi, ahamishwe mara moja.

Walimu hao, wakiongozwa na Katibu wa Tawi la KNUT Makueni Benson Ndambuki, walifika katika ofisi ya Kamishna wa Kaunti na kuwasilisha malalamiko yao.

KNUT imemshutumu Mkurugenzi huyo kwa madai ya kuwatisha na kuwanyanyasa walimu pamoja na wakuu wa shule, na kufanya baadhi ya maamuzi bila mashauriano ya kutosha.

Muungano huo pia umeomba uchunguzi ufanywe kuhusu madai ya matumizi na ukusanyaji wa fedha zinazohusiana na shughuli za elimu.

Malalamiko hayo sasa yamewasilishwa kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi. Ripoti zinasema Mkurugenzi huyo bado hajajibu madai hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *