Waziri wa Elimu, Migos Ogamba, anaongoza kongamano la elimu nchini Kenya, linalolenga kujadili changamoto zinazokabili sekta ya elimu na namna ya kuiboresha.
Kongamano hilo linawaleta pamoja wadau mbalimbali wa elimu, wakiwemo walimu, wazazi, wanafunzi, viongozi na wataalamu wa sekta hiyo.
Mjadala unajikita katika utekelezaji wa mfumo wa CBC, upatikanaji wa walimu, miundombinu ya shule pamoja na ufadhili wa elimu.
Waziri Ogamba anatarajiwa kusikiliza maoni ya wadau na kueleza mikakati ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na yenye usawa.
Kongamano hilo pia linatoa nafasi kwa wadau kupendekeza suluhisho kuhusu changamoto zinazokumba shule na walimu kote nchini.
Serikali imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote katika kujenga mfumo wa elimu unaokidhi mahitaji ya kizazi cha sasa na kijacho.