Walimu wa JSS Embu wasusia kuajiriwa kwa kandarasi

Walimu wa JSS wanaohudumu kwa mafunzo kazini katika Kaunti ya Embu wanataka kuajiriwa kwa masharti ya kudumu na ya pensheni badala ya kandarasi, wakilalamikia malipo ya chini ya takriban Sh17,000 baada ya makato. Wanasema zaidi ya walimu 44,000 wa JSS kote nchini wanapaswa kuthibitishwa kazini mara moja kufuatia uamuzi wa mahakama uliopinga mfumo wa internship.

Walimu hao wameonya kuwa wakipokea agizo kutoka afisi za kitaifa na kaunti, wataanzisha mgomo wa kitaifa ndani ya siku saba utakaosimamisha masomo, ikiwemo shule za senior, kwa mshikamano na walimu wa JSS. Pia wanataka JSS ijitenge kiutawala na shule za msingi ili iwe na usimamizi huru.

Ikiwa ni wiki ambayo wanafunzi wanatarajiwa kurudi shule, walimu wa JSS wakiongozwa na katibu mtendaji wa KUPPET tawi la Meru, Njira Muthoni, wamefanya maandamano ya kusinikiza serikali kuwapatia kandarasi ya kudumu. Bwana njira ameweza kusema masomo haitaendelea kama serikali haitaheshimu uamuzi wa Mahakama Kuu na ile ya Rufaa ambayo ilisema kuajiri walimu na kandarasi ni kutofuata sheria.

‎Zaidi ya hayo ameweza kuomba serikali kutenga pesa na kama hizi pesa haziko kutengenezwe bajeti ya nyongeza ili pesa zipatikane na TSC iweze kuajiri walimu hawa na kama si hivyo hawatarudi shule

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *