Waziri aongoza ushirikishwaji wa umma mradi wa maji Meru

Waziri wa Maji Kenya, Eric Mugaa, ameongoza zoezi la ushirikishwaji wa umma kuhusu mradi wa maji katika eneo la Kiirua, Kaunti ya Meru, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa viongozi na wananchi katika kufanikisha maendeleo.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika Buuri, katika kaunti hio ya Meru, waziri Mugaa alisema juhudi za pamoja kati ya Mbunge wa Buuri, Mugambi Rindikiri, na Mbunge wa kuteuliwa Dorothy Muthoni, ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Maji Bungeni, zimefanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 100 kusaidia mradi huo.

Alieleza kuwa fedha hizo zitaleta nafuu kwa wakazi kwa kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama katika Kiirua na maeneo jirani.

Aidha, Waziri huyo aliwahimiza wakazi wa Meru kushirikiana na serikali ili kuharakisha maendeleo, huku akitoa wito wa kumuunga mkono Naibu wa Rais katika juhudi za maendeleo ya taifa.

Mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha mamia ya familia kwa kuboresha huduma ya maji katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *