Serikali za kaunti zimekubaliana kushirikiana na Serikali Kuu katika kuimarisha vita dhidi ya biashara ya pombe haramu nchini Kenya.
Makubaliano hayo yalifikiwa Oktoba 21, 2026, wakati wa mkutano wa pamoja kuhusu pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya, ulioongozwa na Naibu Rais Kithure Kindiki na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Baraza la Magavana.
Miongoni mwa hatua zilizopendekezwa ni kuanzishwa kwa mfumo wa pamoja wa utoaji leseni kwa biashara za pombe katika kaunti zote, kuimarisha operesheni za kiusalama zinazotegemea taarifa za kiintelijensia na kuimarisha ushirikiano kati ya idara mbalimbali za serikali.
Serikali hizo pia zimekubaliana kupitia upya sheria na kanuni zilizopo, huku wananchi wakihimizwa kushiriki katika kutoa taarifa kuhusu biashara haramu za pombe.
Hatua hizo zinalenga kuvunja mitandao inayohusika na utengenezaji na usambazaji wa pombe isiyokidhi viwango vya afya na usalama, pamoja na kuwalinda watumiaji dhidi ya madhara ya pombe hatari.