Rais Ruto atia saini miswada ya marekebisho ya sheria za ushuru na KRA ya 2026

Rais William Ruto ametia saini miswada miwili ya marekebisho ya sheria za ushuru na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA) kuwa sheria. Miswada hiyo ilisainiwa katika Ikulu ndogo ya Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, Ijumaa, Oktoba 16, 2026.

Sheria ya marekebisho ya ushuru inaendeleza kupunguzwa kwa ushuru wa VAT kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8 kwa kipindi cha siku 90. Hatua hiyo inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya kupanda kwa gharama ya mafuta.

Sheria hiyo pia inarekebisha ushuru wa vifaa vya ujenzi, ikiwemo vigae na vifaa vya usafi.

Kwa upande mwingine, marekebisho ya sheria ya KRA yanalenga kuboresha usimamizi wa mamlaka hiyo na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *