Wasonga ailaumu serikali kwa kutokuwa na nia ya kumaliza mgomo wa wahadhiri

Katibu Mkuu wa Muungano wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu nchini (UASU), Dkt. Constantine Wasonga, ameilaumu serikali kwa kile anachosema ni ukosefu wa dhamira ya dhati ya kumaliza mgomo wa wahadhiri katika vyuo vikuu vya umma.

Wasonga anasema pendekezo la hivi karibuni la serikali kuhusu makubaliano ya pamoja ya mishahara na marupurupu ya wafanyakazi kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2029 halikukidhi matakwa ya vyama vya wafanyakazi.

Mgomo huo unaendelea kufuatia kushindwa kwa mazungumzo kati ya serikali na vyama vya wafanyakazi mnamo Jumatatu, Oktoba 12, 2026. Vyama hivyo vinataka makubaliano ya pamoja ya kazi, CBA, yakamilishwe na kutekelezwa kabla ya wahadhiri kurejea kazini.

Mgogoro huo umeathiri shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma, huku maelfu ya wanafunzi wakikosa masomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *