Papa Leo Kushiriki Chakula na Wahitaji 200 Huko Castel Gandolfo

Papa Leo anatarajiwa kushiriki chakula cha mchana na wahitaji wapatao 200 kutoka Jimbo la Roma katika Borgo Laudato si’, Castel Gandolfo, Jumamosi. Tukio hilo litaanza kwa adhimisho la Ekaristi likifuatiwa na matembezi katika bustani za Borgo Laudato si’ na baadaye chakula cha pamoja na Baba Mtakatifu.

Lengo la shughuli hiyo ni kuonyesha kuwa utunzaji wa mazingira na kuwajali watu walio katika mazingira magumu ni sehemu ya utume mmoja wa Kanisa. Walioalikwa ni maskini, wakimbizi, wahamiaji na watu wengine wanaosaidiwa na parokia, Caritas pamoja na mashirika mbalimbali ya kijamii katika Jimbo la Roma.

Viongozi wa Kanisa wamesema kuwa kukutana kwa Papa na wahitaji kunadhihirisha upendo wa Injili kwa vitendo na kurejesha heshima kwa wale wanaoishi pembezoni mwa jamii. Aidha, waamini wamehimizwa kuendeleza moyo wa ukarimu, mshikamano na kuwakaribisha wote bila ubaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *