Seneta Munyi Mundigi aomba washikadau kusitisha migomo

Seneta wa Embu, Alexander Munyi Mundigi, amewahimiza viongozi wa dini, wazazi, wanafunzi, na walimu kufanya kikao cha dharura kutafuta suluhu ya migomo inayozidi kuongezeka kaunti hiyo.

Mundigi amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya wadau hawa ni muhimu ili kutatua kero zinazosababisha machafuko mashuleni. Hii imejia baada ya shule kadhaa hadi za kutwa kushiriki migomo, na kusababisha uharibifu na kutatizika kwa elimu.

Ameeleza kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee ya kurejesha utulivu wa kimasomo na kulinda mustakabali wa wanafunzi pamoja na mali ya shule mkoani humo. Pia amependekeza kuwe na mafunzo ya mawaidha kwa wanafunzi mara kwa mara, ili wawe waadilifu kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *